Wanaume wasiokuwa kwa mahusiano huteseka sana kuliko kina dada- Utafiti
UTAFITI uliochapishwa kwenye Jarida ya Kisaikolojia na Masuala ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Toronto, unasema kuwa wanawake ambao hawapo katika uhusiano wa kimapenzi huwa na furaha na hawaathiriki kisaikolojia ikilinganishwa na wanaume.
Wanaume makapera huwa wamesononeka na hukabiliwa na changamoto kiasi kuwa wapo kwenye hatari ya kutatizika kisaikolojia.
Utafiti huo uliwashirikisha watu 6,000 ambao ni watu wazima na wametinga umri wa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.: Katika kila swali walipoulizwa, wanawake walijibu kwa kusema walikuwa wakifurahia maisha ya kutokuwa na mpenzi. Hii ni kwa sababu wanawake wengi hawachukulii ngono kama mhimili wa uhusiano.
Isitoshe wanawake walisema kuwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi si muhimu kwao kwa sababu kunatwaa muda mwingi ambao wangetumia kufanya kazi za nyumbani.: Wengine walidai suala la ngono au mapenzi hutumika kuwadhalilisha katika jamii.
Wanawake pia hutumia muda mwingi kuyafuatilia mambo yanayowanufaisha ikilinganishwa na wanaume.
Aidha wanaume ilibanika ndio huwa wanapata manufaa mengi kwenye uhusiano wa kimapenzi kuliko wanawake ndiposa wao huathirika wakiishi maisha ya upweke.
Japo tafiti za awali zilikuwa zimeashiria wanawake ndio walikuwa wakimakinikia sana mahusiano, wameshangazwa na hali kuwa wale ambao hawapo katika ndoa ndio wanafanya vyema katika kutengeneza mali na kujitajirisha.
Kwa upande wao, wanaume ambao wanaishi maisha ya upweke huishia kudhalilishwa hasa katika jamii ambazo zinathamini ndoa na wengine huongezewa majukumu ya kuwajibikia katika familia