Wataalam wahimiza kufua taulo angalau mara mbili baada ya kujipangusa nayo
JE, wewe hufua taulo yako baada ya kuitumia mara ngapi?
Iwapo wewe huoga mara moja kwa siku, basi siku ifuatayo unapaswa kufua taulo yako.
Na iwapo unaugua ugonjwa unaodhoofisha kinga mwili yako au una maambukizi, unapaswa kufua taulo yako muda ukimaliza kujipangusa.
Wataalamu wa afya wanasema kuwa unapojipangusa, unahamisha maelfu ya seli za ngozi pamoja na mamilioni ya vijidudu kama bakteria na fangasi kwenye taulo.
Unapoitumia tena, unamwaga seli zingine na vijidudu hivyo kuunda mazingira mazuri ya vijidudu hivyo kustawi.
Hii ni kwa sababu, taulo hubaki na unyevu kila unapoitumia kujipangusa maji.
Baada ya muda wa kutofua taulo yako, huanza kunuka kama manyoya ya mbwa aliyenyeshewa kwa sababu hushikilia jasho, umajimaji wa mwili, ambayo huliwa na bakteria na fangasi, kisha kutoa harufu hiyo, wataalam hao wanaeleza.