Makala

AMINI USIAMINI: Kuku ni ‘mjukuu’ wa T-Rex

March 28th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA PETER MWORIA

KUKU ndio viumbe wanaoishi ambao ni wa karibu sana na jamii ya viumbe walioangamia duniani walioitwa T-Rex.

Viumbe hao ambao jina lao la kisayansi ni Tyrannosaurus rexwalikula nyama na walitembea kwa miguu miwili, walitoweka duniani kati ya miaka milioni 72 na 66 iliyopita.

Kwa hivyo, unapomuona kuku, jua anafanana na viumbe hao ambao kwa sasa tunawaona tu kwenye picha za kubuniwa.