Bambika

Azziad ajigamba ni Gen Z hodari wa kukoroga lugha ya mama

February 14th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA FRIDAH OKACHI

VIJANA wengi wa kizazi cha sasa almaarufu Gen Z na Millenial, mara nyingi hujifanya hawajui lugha ya kwanza kisingizio kikiwa kwamba “sisi ni born town” kumaanisha wao ni wa mjini.

Mwanahabari na msanii Azziad Nasenya anaona mtazamo huo kuwa hasi.

Kudhihirisha namna alivyo vingwa wa kukoroga kugha ya mama, Azziad alizungumza Kiluhya bila kutatazika.

Kwenye mahojiano na kituo cha PPP TV, alipewa fursa ya kuzungumza lugha ya mama ambapo sharti lilikuwa kwamba hakuna nafasi ya kutapatapa.

“Nimezaliwa na nikalelewa Kaunti ya Kakamega, kwa hakika ninaweza kuzungumza kwa ufasaha lakini nyanya yangu anasema naongea kama vile nina uji wa moto mdomoni,” akasema Azziad.

Mbe uvusuma nindi ighokho, mbeye na nindi itsaara … (nipe ugali na kuku kwa sababu nina njaa),” akasema.

Mahojiano hayo yalishangaza mashabiki wake wanaomfahamu kuwa mzaliwa wa Nairobi na lugha anayozungumza sana ni Kiingereza.

Wengi mtandaoni waliandika jumbe za kumsifia licha ya kujulikana kuzungumza vyema Kingereza na Kiswahili.

Jason Wasena alionya wale ambao hukosa kujua lugha zao za kiasili.

“Epuka watu wanaofikiria kutojua lugha yao ya kiasili ni jambo la kujionea fahari,” alisema Jason.

Naye shabiki mwingine kwa jina Mrs Maggie alichangia akisema kuwa msanii huyo anajivunia lugha yake.

“Anajivunia kabila lake. Waluyha hawafichi utambulisho wao wa kweli kwa sababu wanaupenda na kuuenzi,” akasema Mrs Maggie.

Azziad ambaye huvuma sana TikTok alizaliwa Mumias, lakini akalelewa Kakamega na kisha Nairobi.

Azziad ni mmojawapo wa watengenezaji wa maudhui wenye umaarufu mkubwa.

Wakati wa janga la Covid 19 alitumia mfumo ya kidijitali kusambaza talanta yake ya kunegua.

Mara ya kwanza kutambulika ni kipindi anashiriki kwenye video ya wimbo wa Utawezana wake Mejja akimshirikisha Femi One.

Mwaka 2020 aliigiza kama mwanamke anayeongoza katika safu ya televisheni kwenye Maisha Magic East Africa.

Kwa sasa yeye ni mtangazaji wa redio kwenye kipindi cha asubuhi.