• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Lupita Nyong’o azungumzia ugumu wa kuandaa filamu ya majitu yasiyopenda kelele

Lupita Nyong’o azungumzia ugumu wa kuandaa filamu ya majitu yasiyopenda kelele

NA SINDA MATIKO

MWIGIZAJI staa Lupita Nyong’o amezungumzia ugumu aliokumbana nao kwenye filamu mpya ya kuogofya itakayoachiwa Juni 2024 yenye anwani “A Quiet Place: Day One”.

Kwenye filamu hiyo, jiji la New York linavamiwa na majitu yasiyoona na yasiyopenda kelele hata kidogo.

Licha ya kuwa hayaoni, yana uwezo wa kufuatilia aina yoyote ya kelele na kufanya maangamizi.

Ili kutoboa, inalazimu watu kuishi kama mabubu, jambo ambalo sio rahisi kiuhalisia.

“Nina uhakika matukio ya filamu hii yatawakamata wengi. Nasema hivi maana nimegundua ni jinsi gani ni vigumu kuishi maisha ukiwa kimya. Kibinadamu sio rahisi hivyo hata kuifanikisha hali hii kwenye filamu halikuwa jambo dogo,” anasema Lupita.

Hii itakuwa ni filamu ya tatu kwenye mfululizo wa filamu hiyo ya kuogofya. Toleo la kwanza A Quiet Place lilitoka 2018 kabla ya A Quiet Place: Part II kufuata 2021. Baada ya kufanya vizuri, maprodusa wakaamua kuandaa A Quiet Place: Day One ambapo Lupita atahusika.

Toleo hili linalotarajiwa sokoni Juni 28, 2024, ni simulizi ya matukio yalivyojiri katika siku ya kwanza, majitu hayo yalipovamia ulimwengu yakitokea kusikojulikana.

  • Tags

You can share this post!

Fahamu msikiti maridadi zaidi kisiwani Lamu

Mwalimu ajiua kwa kukataliwa na ex, aacha mke mjamzito

T L