Nazizi afunguka jinsi mwanawe mdogo alifariki wakiwa hotelini Tanzania
NA SINDA MATIKO
MIEZI mitatu baadaye, rapa Nazizi kwa mara ya kwanza amefunguka mazingira yaliyopelekea mwanawe kufariki huku akikana taarifa zilizosambaa.
“Kuna bloga alianzisha uvumi kuhusu ajali ile pasi na kuthibitisha taarifa zile kutoka kwetu. Bloga huyo alidai kuwa mume wangu alikuwa bize kwenye simu ajali ilipotokea. Sio kweli. Ukweli ni kuwa hoteli tulimokuwa ilikuwa na ua mkubwa sana hivyo alimruhusu mwanawe kujiachia. Hakutegemea ajali kama ile ingetokea maana ukubwa wa vyumba vya hoteli ile ulimhakikishia usalama. Ila ikaja kutokea. Mwenzenu mpaka leo hajawahi pata amani,” Nazizi anasema.
Rapa huyo mkongwe alimpoteza mtoto wake Jazeel Adam Disemba 25 mwaka jana baada ya mtoto huo kudondoka kutoka kwenye ua la hoteli moja.
***
Lalama za Wema kuhusu uigizaji wake
Mara ya mwisho yeye kuvalia uhusika ilikuwa kwenye sinema ya Karma iliyokuwa ikipeperushwa na DSTV.
“Mara ya mwisho kuigiza ilikuwa kwenye Karma. Baada ya kutokea kwa mitafaruku kibao na DSTV, jambo hilo lilinitoa kabisa kwenye reli.
Juzi nimeona DSTV walitangaza kuachishwa kazi kwa wale mabosi wawili Babra na Onesmo waliohusika kwenye skendo hizo na sababu ni kwamba walikuwa na nia zao za kujifaidi kutokana na zile kazi ambazo walikuwa wanazipokea na kupitisha kurushwa DSTV,” anasema Wema.
Mrembo huyo anaishtumu DSTV kwa kumvurugia imani yake kwenye uigizaji baada ya skendo hiyo iliyovuruga pia shoo yake hiyo ya karma.
“DSTV wamenirudisha nyuma sana. Nilikuwa nimejitoa sana kwenye Karma ukizingatia kwamba sikuwa nalipwa ninavyostahili.
Waliniahidi vitu vingi na kuniaminisha kuwa nimewekeza kwenye jambo litakalonilitea faida nyingi.” kabisa lakini wapi,” Wema kalaumu.
Staa huyo anasema aliwekeza fedha zake binafsi kwenye shoo hiyo ya Karma ilipochukuliwa na DSTV lakini sakata hizo zikaishia kumvuruga ikiwemo kuikwamiza shoo yake hiyo.
“Ila bado sijaacha kuigiza najua mashabiki wamenimisi ila vitu wakati mwingine hutokea, ila nitarudi.”