• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Octopizzo: Wasanii wa sasa hawatoboi kisa Insta na TikTok

Octopizzo: Wasanii wa sasa hawatoboi kisa Insta na TikTok

NA SINDA MATIKO

RAPA Octopizzo anadai kuwa sababu ya kizazi cha sasa cha wasanii kushindwa kutamba kwa muda mrefu ni uwepo wa mitandao ya kijamii.

Octopizzo anasema kwamba uwepo wa mitandao ya kijamii umewafanya wasanii wa kizazi cha sasa kuwa wazembe na ndio maana wanashindwa kudumu kwenye muziki.

“Kama vipaji vipo vya kutosha sana, kuna zaidi ya Octopizzo 1,000 kule mtaani ila nahisi kizazi cha wasanii wa sasa hakipendi kujituma kama enzi sisi tunatoka. Na hii ni kwa sababu ya uwepo wa mitandao ya kijamii,” Octopizzo anasema.

“Yaani mtu anaona akishaachia hiti moja akaiposti YouTube, Instagram na Twitter basi ndio kafika. Akishafanya hivyo anakaa hata mwaka mzima bila kuachia ngoma nyingine…anasubiri mafanikio yatamkuta,” anaongeza.

Akilinganisha na wakati yeye anaanza, rapa huyo anasema kizazi chake kilikuwa cha kujituma kwelikweli na ndio sababu mpaka sasa, yeye na wenzake kama Khaligraph Jones, na King Kaka bado wanazidi kutesa kwenye gemu zaidi ya miaka 10 sasa ukilinganisha na wasanii wengi waliobuka miaka mitano au mitatu iliyopita lakini ghafla nyota yao ikazima.

“Kipindi chetu ulikuwa unaachia kwanza mixtapes, halafu sasa ndio unaangusha zile singo. Ukitoka pale ndio unawaza sasa kuachia albamu, lakini hawa wa sasa hawafanyi hivyo. Akitoa hiti moja ndio basi anaona ameshafika. Hii ndio sababu wanafulia mapema,” anadai Octopizzo.

  • Tags

You can share this post!

Binti ajisalamisha kortini kushtakiwa kwa kughushi wosia wa...

Wakazi wa Witeithie waandamana kwa ‘kubaguliwa...

T L