• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 10:27 AM
Staa wa ‘Mali Safi Chito’ apambania hakimiliki ya wimbo wake

Staa wa ‘Mali Safi Chito’ apambania hakimiliki ya wimbo wake

NA WANDERI KAMAU

Mwanamuziki huyo alisema kundi hilo limekuwa likizima sauti za wimbo huo kwa kwenye video za watu wanaotumia katika mtandao wa Tiktok.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Taifa Leo mnamo Alhamisi Machi 7, 2024, Marakwet Daughter alisema kuwa kundi hilo tayari limeanza kudai ndilo linalomiliki  wimbo huo.

“Kando na kuniambia ndilo lenye hakimiliki ya wimbo huo, kundi hilo limekuwa likizima sauti za nyimbo zangu zinazotumiwa na mashabiki wangu kujiburudisha katika mtandao wa Tiktok. Hilo ni jasho langu. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba hakuna yeyote atakayetumia njia ya mkato kuninyang’anya hakimiliki ya wimbo huo,” akasema Marakwet Daughter.

Alisema ana hasira.

Mwanamuziki huyo alidai kuwa kundi hilo limekuwa likipakia wimbo huo katika akaunt tofauti za YouTube bila ruhusa yoyote kutoka kwake.

“Niko tayari kuchukua hatua yoyote kutetea nyimbo zangu,” akasema.

Kauli ya mwanamuziki huyo inajiri siku chache baada yake kutoa onyo kwa wachezaji santuri (DJs), ambao wamekuwa wakiweka wimbo huo  kwenye akaunti zao za YouTube bila kibali kutoka kwake.

“Wachezaji santuri huwa nguzo muhimu sana katika kuusambaza wimbo kwa mwanamuziki kwa waimbaji wake. Hata hivyo, hilo halimaanishi wauweke wimbo huo kwenye akaunti zao za YouTube ili kupata pesa kupitia wimbo au nyimbo zangu,” akasema.

Mwanamuziki huyo alijizolea umaarufu mwaka uliopita kupitia wimbo huo, baada ya Wakenya kuushabikia sana kupitia mitandao ya kijamii.

Kufikia sasa, wimbo huo una zaidi ya mitazamo milioni nane katika mtandao wa YouTube.

Kabla ya wimbo huo kuwa maarufu, mwanamuziki alisema ilimchukua karibu miaka 20 ili kutambulika.

“Nimekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa karibu miaka 20. Kabla ya wimbo huo kuwa maarufu, si wengi walinitambua. Nilikuwa nimeteseka sana,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Siasa zatingika Rais Ruto akipendekeza mgombea mwenza awe...

Nyakang’o amulika serikali kwa kutumia Sh70.41bn bila...

T L