Faida ya kuvaa soksi
Na MARGARET MAINA
MIGUU ni sehemu mojawapo inayotoa jasho sana hivvo ni vyema kuhakikisha inakuwa mikavu kuzuia ukuaji wa bakteria au fangasi.
Wengine wetu tunajua umuhimu wa soksi na wengine hatuvai.
Hii ni kwa kina dada pia wanaovaa viatu kama raba. Ni vyema sana kufahamu kwa nini tunavaa soksi na muda mwingine soksi gani tuvae.
Kuzuia magonjwa ya ngozi miguuni
Kuvaa soksi kutakukinga na maradhi haya ya fangasi na bakteria.
Epuka harufu mbaya ya miguu
Kwa kweli hii ni kero kwako na wanaokuzunguka. Usipovaa soksi, jasho lote la miguu litaenda kwenye viatu na hivyo viatu vitaanza kutoa harufu. Soksi hunyonya lile jasho na huzuia harufu hiyo.
Lainisha ngozi ya miguu yako
Nani hapendi miguu laini? Kina dada huenda kusuguliwa miguu saluni, lakini wakirudi nyumbani kama sakafu ni ngumu, ni muhimu wazingatie kuvaa soksi nyepesi na safi miguu iwe laini. Baadhi ya viatu pia vina vikanyagio vigumu kwa chini na hii ni hatari.
Kupunguza maumivu miguuni
Hii hasa ni kwa watoto wadogo. Tuwazoeshe mapema kuvaa soksi. Mtoto anapotembea nyumbani, mara atakanyaga maji, mara vitu vya ncha kali na kadhalika. Pia kuna viatu akivaa bila soksi lazima ahisi maumivu. Ni muhimu kuhakikisha unatu
Kupata joto nyakati za baridi
Wale wa maeneo yaliyo na baridi ni muhimu wafahamu soksi za kutosha zinafaa miguuni na glavu mikononi.