• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
SOKOMOKO: Kujitetea kwa Murkomen kuhusu ajali barabarani kwakera Wakenya

SOKOMOKO: Kujitetea kwa Murkomen kuhusu ajali barabarani kwakera Wakenya

WIKI iliyoisha, Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen alijipata motoni alipojaribu kujiondolea lawama kuhusiana na ongezeko la maafa kutokana na ajali za barabarani nchini.

Wakitumia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, Wakenya walimponda, wengine wakimtaka ajiuzulu ikiwa amelemewa na kazi.

“Ukiniuliza anayepasa kubeba lawama ni Waziri Murkomen. Michuki (John Michuki waziri wa zamani wa uchukuzi) aliposhikilia usukani, alionyesha ukali wake kwa vitendo. Hakulaumu raia bali alipambana vikali na madereva watundu na wavunjaji sheria,” anasema Duke Macharia kupitia mtandao wa X.

Kwa upande wake, @Papawetu anasema hivi: “Ni wazi kuwa Murkomen ameshindwa kazi na hana budi kujiuzulu ili mtu mwingine apewe kazi hiyo. Kwa hakika hamna uhaba wa watu wanaoweza kutekeleza kazi hiyo.”

Mnamo Jumatano, Murkomen alisema hafai kulaumiwa kwa ongezeko la ajali za barabarani ambazo tangu Januari zimeangamiza watu 1,214.

Badala yake aliwataka raia kuelekeza kero na lawama zao kwa Idara ya Polisi wa Trafiki na Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Barabarani (NTSA) akisema asasi hizo mbili ndizo zinawajibika na usalama barabarani.

“Sio sawa kwa kulaumu Waziri wa Uchukuzi kila mara ajali inapotokea….. eti wanauliza, wapi waziri. Watu hata huingia ndani ya matatu iliyobeba abiria wengi kupita kiasi na kuchukua video na picha huku wakiuliza wapi Murkomen. Murkomen amefeli!” Waziri Murkomen akafoka kwenye kikao na wanahabari afisini mwake Nairobi.

Lakini waziri huyo, ambaye mwaka jana alitangaza kuwa angelala katika uwanja wa ndege wa JKIA kuhakikisha nguvu za umeme hazipotei, anaonekana kusahau kuwa NTSA iko chini ya Wizara yake.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa mkuu wa ulanguzi wa mihadarati anaswa

Kama mna nguvu mtufikie basi, Man City waashiria Arsenal na...

T L