• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
Uchaguzi wa mashinani unavyotishia UDA, ODM

Uchaguzi wa mashinani unavyotishia UDA, ODM

Nyadhifa

Katika Kenya Kwanza uchaguzi umezua tumbojoto kufuatia kubuniwa kwa nyadhifa za manaibu kadhaa wa kiongozi wa chama huku Naibu Rais Rigathi Gachagua na wafuasi wake wakilalamika kuwa hatua hiyo inalenga kumtoa pumzi asiwe na usemi mkubwa chamani na kumnyima nafasi ya kuwa mrithi wa Rais Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2032. Inasemekana kuwa Bw Gachagua amepiga kambi katika makao makuu ya chama cha UDA kwa kile wachanganuzi wa kisiasa wanasema ni juhudi za kulinda maslahi yake katika uchaguzi huo.

“Gachagua anajua kuwa uchaguzi huo utaathiri sio tu wadhifa wake chamani lakini pia nafasi yake ya kuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao na ya kurithi urais. Anacholenga ni kuhakikisha kwamba wengi watakaochaguliwa katika matawi watakuwa washirika wake ili aweze kuthibiti chama kuanzia mashinani,” asema mchanganuzi wa siasa Jacob Wasike.

Kulingana naye, uchaguzi wa mashinani wa UDA unaweza kuzua mgawanyiko baridi katika ya Mlima Kenya na Rift Valley ambako viongozi wake wakuu Bw Gachagua na Rais Ruto wanatoka.

Tumbojoto

“Kinachomtia tumbojoto zaidi Bw Gachagua ni nyadhifa tatu zaidi za manaibu wa kiongozi wa chama ambazo bila shaka zitamtoa pumzi hasa ikiwa ni kweli Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi ataunganisha chama chake na Amani National Congress (ANC) na UDA,” aeleza Wasike.

Hii, asema, itakuwa pigo kwa Gachagua ambaye hatakuwa mgombea mwenza wa moja kwa moja wa Rais Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027 na kupunguza nafasi ya kurithi urais katika uchaguzi mkuu wa 2032 kwa tiketi ya UDA. Wasike anabashiri kuwa uchaguzi huo utafifisha ukuruba katika ya Ruto na Gachagua.

Katika ODM uwezekano wa Raila kuchaguliwa mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC ) unatishia kugawanya chama hicho kilichodumu kwa miaka mingi nchini tangu kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi nchini.

Manaibu wawili wa chama hicho Hassan Joho na Wycliffe Oparanya ambao ni wandani wa miaka mingi wa Odinga, wanawania kuchukua nafasi ya waziri mkuu huyo wa zamani. Wote wawili wana azima ya kugombea urais na duru zinasema kila mmoja wao amekuwa akifanya kampeni za chini na kufadhili washirika kuchaguliwa katika uchaguzi wa mashinani wa chama.

Huku Oparanya na Joho wakilumbana kuhusu anayefaa kurithi Odinga kama kiongozi wa ODM, wanasiasa kutoka Nyanza, wanahisi kuwa hawafai kupoteza uongozi wa chama hicho cha chungwa.

Nyanza ni ngome ya kisiasa ya chama hicho na nyumbani kwa Bw Odinga.

Umoja

Katika mkutano wa Baraza Kuu la chama wiki hii, Bw Odinga alihimiza umoja kudumishwa katika chama hicho hata akiondoka na akaashiria kuwa yuko tayari kupisha viongozi vijana kukisimamia mradi tu kisisambaratike.

Odinga alisema kuwa hawezi kuongoza chama milele na kusema hakifai kuzama akiondoka. Kulingana na mdadisi wa siasa Dkt Emmanuel Donga, uchaguzi wa mashinani wa vyama vya UDA na ODM unaweza kuvififisha, kuvipomoromosha na kuvitia nguvu.

“Hii ni kwa sababu ya mivutano ya kimaslahi inayojitokeza,” asema.

  • Tags

You can share this post!

Nyota Kaka alivyoachwa na mke kwa kuwa ‘mzuri...

Masaibu bondeni Kerio yahusishwa na nguvu za giza

T L