Makala

Jinsi ya kuandaa juisi ya mua

December 15th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Wanywaji: 3

Vinavyohitajika

  • miwa miwili na zaidi
  • maji jagi moja
  • tangawizi (sio lazima kama hauna)
  • vijiko vitatu vya juisi ya limau
  • chujio
  • glasi tatu

Maelekezo

Chukua miwa yako uliyo iandaa na kuyaosha yawe safi kabisa.

Menya maganda ya miwa hiyo au ondoa maganda ya miwa hiyo.ilikusudi mua wetu ubaki ni mweupe usiwe na ganda hata moja.

Kata miwa hiyo katika vipande vipande.

Hakikisha vipande hivyo vya mua havizidi ukubwa wa inchi moja kwani vinaweza kuharibu mapanga ya blenda yako.

Chukua vipande hivyo vya miwa kisha changanya na nusu kikombe cha maji kisha viweke katika blenda,pia changanya na tangawizi kama utapenda kisha washa blenda yako na hakikisha unasaga juisi yako mpaka ukaona kua hakuna vipande vipande vya miwa.

Sasa baada ya kuona juisi yako imekwisha sagwa vizuri chukua chujio au kitambaa kisafi kisha chuja juisi yako.

Na hapo ndio utakuwa tayari umeshaandaa juisi ya mua.

Unaweza ukanywa pamoja na wenzako na mukafurahia.

Faida za juisi ya mua

Juisi ya mua ina sukari ambayo kwa lugha ya Kiingereza tunaita (sucrose sugar).

Hi sukari husaidia katika kuipa nguvu mwili.kwani ni sawa na unapo kula glucose basi hujisikia mchangamfu ndivyo hivyo utakapo kunywa juisi ya miwa utajisikia mchamfu na nguvu ya mwili wako itarejea.

Kama hua unajisikia umechoka jitahidi uandae juisi ya mua na unywe na utajisikia vizuri.

Pia juisi hii ya miwa ina madini mengi ya chuma kama zinki, magnesiumu, calcium na chuma haya husaidia katika utengenezaji wa damu na kupambana na magonjwa mbalimbali.