• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Jinsi ya kuhifadhi mboga na matunda katika jokofu

Jinsi ya kuhifadhi mboga na matunda katika jokofu

Na MARGARET MAINA

[email protected]

OSHA mboga na matunda ili kuondoa uchafu.

Kumbuka kuna baadhi ya mboga ambazo ukiziosha zinaharibika haraka hivyo basi zioshe tu sehemu ya mizizi.

Kausha mboga na matunda. Chukua taulo safi ya jikoni na ukaushe mboga na matunda. Hakikisha ni kavu kabisa. Ni muhimu kukausha kwani uwepo wa unyevuunyevu katika mboga na matunda hutengeneza mazingira mazuri ya ukuaji wa bakteria na fangasi.

Weka mboga na matunda ndani ya mifuko ya plastiki na kisha uifunge mifuko hiyo. Ni bora zaidi ukitumia mifuko ya plastiki inayoweza kutumika tena na tena – Ziploc bags – ambayo inaonyesha (transparent).

Mifuko hii hupatikana kwa wingi sana madukani; chagua ukubwa unaotaka kutegemea na unataka kufunga ama mafungu makubwa au madogo kiasi gani.

Toboa mfuko wenye mboga au matunda. Toboa toboa matundu mengi ya kutosha katika mfuko huo wenye mboga na matunda hasa sehemu za chini. Hii ni kuruhusu hewa ya baridi kuingia ndani ya mfuko na kuzifikia mboga au matunda moja kwa moja na kwa wakati huo huo kuzuia aina yoyote ya unyevuunyevu kufikia mboga na matunda ndani ya mfuko.

Weka mifuko ya mboga na matunda katika jokofu kwa mpangilio mzuri. Zingatia upangaji ili kunusuru vitu kama nyanya na ndizi mbivu visipondeke.

Ushauri

Kutokana kwamba watu wengi huzembea au hushindwa kukausha mboga na matunda baada ya kuosha na kisha kufanya viharibike mapema, waweza kuacha kuosha matunda na mboga hizo bora tu uzifute ili kuondoa ule uchafu wa juu na uendelee kuzifunga.

Ukiamua kutokuosha, hakikisha kila mwana familia anajua kuwa mboga na matunda ndani ya jokofu havijaoshwa ili waoshe kabla ya kutumia au kula.

 

You can share this post!

Wanafunzi wa Kenya waliokwama Sudan kurudishwa nyumbani

SIHA NA LISHE: Namna ya kuondoa asidi inayosababisha...

adminleo