Jinsi ya kukuza furaha miongoni mwa matineja
KUJIHISI vizuri na kujenga urafiki ni malengo ya watu wa rika lolote.
Lakini kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 9 hadi 12, wanaojulikana kama matineja, malengo haya yanaweza kuwa na maana ya kipekee.
Katika kipindi hiki kigumu cha mpito kati ya utoto na ujana, urafiki wa karibu na ustawi ni muhimu sana.
Kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la Public Library of Science, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha California, Riverside waligundua kuwa watoto wanaofanya matendo ya wema kwa wengine sio tu huwa na furaha zaidi, bali pia huwa maarufu zaidi miongoni mwa wenzao.
Watoto zaidi ya 400 walishiriki katika utafiti huu uliotekelezwa katika madarasa 19 tofauti.
Wanafunzi waligawanywa katika makundi mawili.
Kila wiki kwa muda wa wiki nne, nusu ya wanafunzi waliombwa kufanya matendo matatu ya wema kwa yeyote waliomtaka.
Nusu nyingine waliombwa kutembelea sehemu tatu wanazofurahia.
Baada ya wiki nne, watoto waliulizwa kueleza kuhusu kiwango chao cha furaha na mahusiano yao na wenzao.
Watafiti waligundua kuwa, ingawa makundi yote mawili yaliongeza hali ya ustawi kupitia shughuli zao, watoto waliotekeleza matendo ya wema walikuwa na furaha zaidi kuliko wale waliotembelea sehemu nzuri.
Zaidi ya hayo, watoto hao pia walikubalika zaidi na wenzao.
“Ujumbe unaopatikana hapa ni kwamba kufanya matendo ya wema kuna uwezekano wa kuleta faida mbalimbali. Kwanza, kufanya mambo mazuri kwa wengine kunahisi vizuri. Pili, hisia nzuri huongeza hali ya ustawi. Tatu, watu wanapohisi vizuri, wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuwatendea wengine wema,” asema mtaalamu wa malezi Debbie Glaussier.
Waandishi wa utafiti huu wanasema kukubalika kwa watoto miongoni mwa wenzao kwa watoto kunahusiana sio tu na mafanikio makubwa kitaaluma, bali pia hupunguza uwezekano wa kudhulumiwa au kunyanyaswa.
Wanaeleza: “Utafiti wetu unaonyeesha kuwa kufanya mazuri kwa wengine huwanufaisha wale wanaotoa, kwa kuwapatia sio tu ustawi bora bali pia umaarufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa furaha na kukubalika miongoni mwa wenzao, ni jambo la kufurahisha kuwa tuliweza kubaini yote mawili kwa vijana wadogo kupitia shughuli rahisi ya kijamii yenye manufaa.”
Utafiti huu ulifanywa katika mazingira ya shule, na waandishi wanawahimiza walimu na wasimamizi wa shule kuingiza mara kwa mara shughuli za kijamii