Makala

Jinsi ya kutengeneza kinywaji 'dawa'

November 19th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na DIANA MUTHEU

[email protected]

KINYWAJI maarufu cha ‘dawa’ kinatambulika kwa kusaidia kupunguza makali ya mafua.

Ni rahisi kutengeneza kinywaji hiki na mtu yeyote yule anaweza kujitengenezea nyumbani na kujiburudisha. Zaidi, wanaoinywa si watu wenye mafua pekee.

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Vinavyohitajika

  • Limau 2
  • Maji kikombe 1
  • Asali kijiko 1 cha sukari
  • Tangawizi kijiko 1
  • Karafuu chembe 5
  • Mdalasini kipande 1
  • Kichungi
Vinavyohitajika kutengeneza kinywaji ‘dawa’. Picha/ Diana Mutheu

Jinsi ya kutengeneza

Osha viungo vyako vizuri, kamua juisi kutoka kwa limau yako kisha usage tangawizi yako.

Chemsha maji kisha uongeze karafuu pamoja na mdalasini. Ache vichemke pamoja kwa dakika mbili.

Maji yaliyo na baadhi ya viungo yakichemka. Picha/ Diana Mutheu

Ongeza juisi ya limau na tangawizi yako, kisha uongeze asali. Koroga kisha uiache ichemke kwa muda wa dakika mbili.

Tumia kichungi kuondoa vipande vikubwa vya viungo ulivyotumia kuandaa kinywaji chako. Jiburudishe.