Kajala: Sitajisamehe kwa kurudia Harmonize
MWIGIZAJI Frida Kajala amekiri waziwazi kwamba kamwe hawezi kujisamehe kwa kile kitendo cha yeye kurudiana kimapenzi na mwanamuziki Harmonize, licha ya zile fedheha zote alizozipata.
Ikumbukwe kuwa Frida alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Harmonize kwa zaidi miaka miwili.
Hata hivyo, wakati wakiwa kwenye mahusiano hayo, Harmonize alianza kumnyemelea binti yake Frida, soshiolaiti maarufu Paula Kajala kiasi cha kufikia kwa mwanamuziki huyo kuanza kumtupia picha zake za utupu kama njia ya kujaribu kumshawishi kuanzisha mahusiano ya kisiri na yeye.
Zogo hilo lilizua mjadala mkubwa sana na licha ya Frida kuamua kumdampu Harmonize baada ya tukio hilo, aliishia kumrudia baada ya jamaa kumbembeleza sana.
Hata hivyo, penzi lao halikudumu sana na wakaishia kuachana miezi michache baada ya kurudiana.
“Tena baada ya Harmonize kunifanyia tukio zito, nikamrudia mwanamume ambaye alidiriki kumtumia utupu wake mwanangu. Kila nikikumbuka naona nilijali sana mapenzi kuliko mtoto wangu na hilo jambo siwezi kujisamehe kamwe.”