• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Kizaazaa wakongwe walioshtakiwa kuwa Mungiki wakiimba nyimbo za ukombozi

Kizaazaa wakongwe walioshtakiwa kuwa Mungiki wakiimba nyimbo za ukombozi

Na MWANGI MUIRURI

KULIZUKA kizazaa katika mahakama ya Murang’a mnamo Februari 5, 2024 wakati wazee 21 walioshtakiwa kuwa wafuasi wa kundi haramu la Mungiki walipoanza kuimba nyimbo za ukombozi mbele ya hakimu.

Wazee hao wa kati ya miaka 90 na 67 walikamatwa mnamo Desemba 31, 2023 katika makao ya Mukurwe wa Nyagathanga unaokisiwa kuwa kiini cha jamii ya Agikuyu.

Kwa mujibu wa wanautamaduni wa jamii hiyo, ni katika makao hayo ambao Mzee Gikuyu alikuwa akiishi na mke wake kwa jina Mumbi na ambao walizaa wasichana tisa.

Wanane kati ya wasichana hao husemwa ndio waliolewa na wanaume na kukazuka Koo za jamii hiyo.

Haieleweki vyema katika hadithi hiyo kule Gikuyu na Mumbi walikuwa wametoka na pia kwenye wanaume wa kuoa wasichana hao walitoka.

Mbele ya Hakimu E.M Nyaga, washukiwa hao waliokuwa wakiwakilishwa na mawakili Ndegwa Njiru, Jeremiah Kioni na Kinuthia Mwangi walianza nyimbo na kusababisha kikao hicho kuahirishwa kwa dakika 20.

Ilibidi kesi hiyo iahirishwe hadi Jumatano baada ya upande wa mashtaka kusema haukuwa tayari na mashahidi.

Hakimu Nyaga aliutaka upande wa mashtaka ukubalie mkondo wa kisheria kufanya kazi.

Wakati huo huo mzee wa miaka 70 katika Kaunti ya Kirinyaga ameripotiwa kuua kwa kumdunga kisu mwanawe wa kiume wa miaka 32 baada ya mzozo wa urithi wa shamba.

Ripoti ya polisi inaelezea jinsi James Muobe Njagi alipigwa kisu rohoni na babake katika Kijiji cha Karumandi.

Kisa hicho cha Jumapili kiliishia mwili wa marehemu kupelekwa mochari ya Kerugoya huku mshukiwa akitiwa mbaroni.

Polisi walisema mzee huyo atashtakiwa kwa mauaji.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Mfalme Charles aahirisha shughuli rasmi baada ya...

Je, unajua utaratibu wa kumuoa msichana wa Kikikuyu?

T L