Makala

LISHE: Jinsi ya kuandaa mlo wa ndizi za kukaanga kwa rosti ya nyama na kachumbari ya parachichi

November 6th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na MARY WANGARI

LEO hii tutaandaa ndizi za kukaaga kwa mchuzi wa nyama ya ng’ombe na kachumbari ya parachichi.

Viungo unavyohitaji

8 ndizi kubwa za mzuzu (itategemea na idadi ya unaowaandalia chakula).

1 kijiko cha chumvi

1 kilo ya nyama ya ng’ombe

Mafuta ya kupikia

4 karoti kubwa zilizosafishwa

4 vitunguu maji vikubwa

1 kijiko cha tangawizi iliyosagwa

2 pilipili manga

2 parachichi zilizoiva

2 nyanya kubwa zilizoiva

Kipande cha tango

1 limau

Maandalizi ya ndizi za kukaanga

Osha ndizi kisha uzimenye bila kuzikatakata.

Zipake chumvi

Zichome ndizi kwa mafuta mengi yaliyoshika moto kwenye sufuria.

Hakikisha moto ni wa wastan ili kuepuka ndizi kuungua.

Maandalizi ya nyama

Tia nyama kwenye sufuria safi weka maji kiasi na ujike mekoni.

Ongeza tangawizi, majimaji ya limau chumvi kiasi na pilipili kisha ufunike na uache itokote.

Ikisha iva na kuwa laini, ikaange kwa kutia kitunguu maji ulichokatakata vipande vidogovidogo, kitunguu saumu kilichpondwapondwa.

Koroga mchuzi huo na kisha uongeze karoti zako ulizoosha na kukwangura huku baadhi ukizikatakata vipande vidogo vidogo.

Ongeza maji kiasi na kuacha itokote kwa muda kisha uepue ikiwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kuandaa kachumbari ya parachichi

Sawa na maandalizi ya kachumbari nyingine yoyote, osha nyanya, kitunguu maji kisha uvikatekate vipandevipande.

Kwangura tango, katakata parachichi na kisha uchanganye viungo vyote pamoja.

Unaweza pia ukaongeza pipili hoho, karoti na viungo vinginevyo kulingana na jinsi unavyopenda kachumbari yako iwe.

Ongeza chumvi kiasi na unyunyuzie majimaji ya limau na kachumbari sasa tayari kwa kuliwa.

[email protected]