• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
LISHE: Maziwa mgando yana manufaa mwilini

LISHE: Maziwa mgando yana manufaa mwilini

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MTINDI unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kwa sababu una virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.

Mtindi ni chanzo kizuri cha ‘Calcium’, ‘Phosphorus’, ‘Riboflavin (vitamin B2), ‘Iodine’, ‘vitamin B12’, ‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’, ‘Potassium’ na ‘Molybdenum’.

Mbali ya virutubisho hivyo, ndani ya mtindi kuna ‘bakteria hai’ ambao ni muhimu kiafya katika mwili.

Kinga kwa wanawake

Mtindi una uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (vaginal infections). Wanawake wenye magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, wanapaswa kutumia mtindi kiasi cha pakiti moja kila siku kwa muda wa miezi sita. Maambukizi waliyokuwa nayo wanawake hao kabla yatatoweka.

Huondoa lehemu mbaya mwilini

Katika hatua nyingine, mtindi umeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini, na wakati huo huo kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini. Hii inamaanisha kuwa, ikiwa mtindi unaondoa lehemu mbaya, mtumiaji anajiepusha pia na hatari ya kukumbwa na tatizo la shinikizo la damu.

Kusaidia mmeng’enyo wa chakula

Kama unapata shida ya kupata choo, basi mtindi unaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine. Viritubisho vilivyomo kwenye maziwa (probiotics) husaidia sana kupunguza kukosa choo pia huzuia kuharisha.

Kupunguza uzani

Mtindi una kiwango kikubwa cha protini na protini ni muhimu sana katika kudhibiti hamu kubwa ya kula kwas ababu wakati mwingi utakuwa huhisi njaa.

Mtindi pia ni kinywaji kizuri sana kutumia mara tu baada ya kufanya mazoezi. Kuna watu wengi huwa wanatumia protini shake kama kinywaji baada ya mazoezi na ukweli ni kwamba hizi shake nyingi ni bei ghali sana kwa hiyo mtindi unaweza kuwa suluhisho lako kwani una uwiano mzuri wa protini na wanga.

You can share this post!

Taasisi ya kozi za ufundi ya miaka 99 ambayo ilikuwa gereza...

Elfsborg na AIK wanazochezea Wakenya zaandikisha matokeo...

adminleo