Makala

LISHE NA AFYA: Jinsi ya kuandaa smoothie ya stroberi na ndizi

January 10th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

SMOOTHIE ya ndizi na maziwa ina virutubisho vingi mwilini kama protini, vitamini, na madini ya chuma.

Pia inakupa nguvu na kulainisha ngozi ya mwili, kujenga mifupa iwe imara na faida nyinginezo nyingi.

Muda wa kuandaa:  Dakika 10

Wanywaji: 2

Ndizi. Picha/ Margaret Maina

Vinavyohitajika

  • vikombe 2 vya stroberi
  • ndizi 2
  • vikombe 1½ maziwa
  • kikombe 1 mtindi
  • mdalasini kijiko 1
  • asali kijiko 1
Smoothie ya ndizi na stroberi. Picha/ Margaret Maina

 

Maelekezo

Osha na uyakate matunda.

Weka matunda kwenye mfuko wa kuwekea chakula kwenye jokofu. Funga, hifadhi matunda kwenye jokofu.

Ukiwa tayari kutumia, weka maziwa, mtindi na matunda yaliyoganda kwenye blenda au mashine ya kusagia chakula.

Saga hadi yalainike vizuri huku ukiweka asali

Furahia kinywaji chako.