Makala

LISHE: Njugu karanga za kutumbukiza katika yai lililokorogwa

October 6th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 5

Muda wa mapishi: Dakika 15

Walaji: 5

Vinavyohitajika

  • karanga kilo 1
  • mayai mawili
  • mafuta ya kupikia
  • sukari vijiko 5
  • unga wa ngano kikombe kimoja
  • chumvi

Maelekezo

Chukua yai, pasua na koroga kwenye chombo safi.

Chukua karanga na ziweke kwenye chombo ulicho korogea mayai. Changanya kwa kutumia mikono.

Weka chumvi kidogo, changanya vizuri, weka sukari changanya, mimina unga wa ngano, changanya vizuri.

Weka mafuta katika chombo cha kupikia katika meko hadi yapate moto.

Chota karanga kwa kutumia kijiko kikubwa na weka kwenye chombo chenye mafuta kisha zigeuze bila kuacha hadi utakapoona zimebadilika rangi kuwa kahawia.

Tumia kijiko kikubwa kuziepua na weka kwenye chombo safi cha wazi ili zipoe.

Funga kwenye vifuko vidogo na zihifadhi pahala safi tayari kwa kula au zipakue jinsi upendavyo.