• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
LISHE: Uokaji wa keki ya chokoleti na ndizi

LISHE: Uokaji wa keki ya chokoleti na ndizi

Na MARGARET MAINA

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 60

Walaji: 4

Vinavyohitajika

• unga wa ngano vikombe 2

• sukari kikombe 1

• ndizi vipande 2 vilivyoiva vizuri

• mayai 2

• mafuta ya kupikia au siagi kikombe ½

• chumvi kijiko 1 kidogo

• kikombe 1½ maziwa

• unga wa kuokea kijiko 1 kidogo

• kikombe ½ cha kakao ya kuokea

• ladha ya vanilla kijiko 1 kikubwa

Maelekezo

Washa ovena na dhibit joto hadi nyuzi 350. Acha ipate moto.

Kwenye bakuli kubwa, changanya siagi na sukari hadi viwe laini.

Ongeza mayai; moja baada ya lingine. Pasua kisha uyachanganye vizuri.

Kwenye chombo tofauti, changanya unga wa ngano, kakao, vanilla, baking soda na chumvi. Koroga vizuri.

Ongeza mchanganyiko huu kwa ule wa sukari na siagi.

Kwenye chombo kingine, zibonde ndizi hadi ziwe laini kisha ziweka kwenye mchanganyiko wa awali.

Ongeza maziwa kiasi kwenye mchanganyiko huku ukiendelea kukoroga.

Paka mafuta na unga kwenye chombo utakachotumia kuokea. Mimina mchanganyiko kwenye chombo cha kuokea. Weka kwenye ovena na uoke kwa muda wa saa moja.

Keki ya chokoleti na ndizi. Picha/ Margaret Maina

Muda huo ukikamilika keki iko tayari. Ikishapoa, furahia kwa maziwa baridi au kinywaji chochote utakachopenda.

Uwepo wa chokoleti unafanya keki hii ivutie macho huku vanilla ikiipa harufu nzuri na ladha tamu.

You can share this post!

Ochan, Sichenje watia saini kandarasi mpya Ingwe huku...

Maombi ya kuondoa mkosi wa ajali za mara kwa mara yafanyika...