• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Helb na KUCCPS kuunganishwa kuzaa taasisi moja

Helb na KUCCPS kuunganishwa kuzaa taasisi moja

NA DAVID ADUDA

BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu (Helb) na Halmashauri ya Kuwateua Wanafunzi Kujiunga na Vyuo Vikuu na Vyuo Anuwai (KUCCPS), zitaunganishwa na kuwa taasisi moja, kwa mujibu wa rasimu ya sheria iliyopendekezwa na Wizara ya Elimu.

Tayari, mswada huo umetolewa kwa umma ili kuwapa wananchi nafasi ya kutoa maoni yao.

Mswada huo unapendekeza kubuniwa kwa Halmashauri ya Ufadhili na Usimamizi wa Elimu Anuwai (Tepfa), ambayo jukumu lake litakuwa kuwasajili wanafunzi katik taasisi za mafunzo anuwai.

Halmashauri hiyo pia itakuwa ikitoa mikopo na ufadhili wa elimu kwa wanafunzi katika taasisi hizo.

Pia, itatoa miundomsingi ya ufadhili kwa taasisi hizo.

Kwa sasa, kuna taasisi mbili huru zinazoendesha majukumu hayo mawili—Heln na KUCCPS.

Bodi ya HELB huwa inatoa mikopo na basari za elimu kwa wanafunzi, huku KUCCPS ikiwasajili wanafunzi kujiunga na vyuo vikuu na vyuo anuwai kulingana na kozi walizoteuliwa kufanya.

Taasisi nyingine ni Bodi ya Ufadhili wa Vyuo Vikuu (UFB) ambayo hutoa ufadhili kwa vyuo vikuu; na Bodi ya Ufadhili wa Taasisi na Vyuo vya Kiufundi (TVETFB), ambayo iliitarajiwa kutoa ufadhili kwa taasisi za kiufundi, japo bado haikuwa imeanza kutekeleza jukumu hilo.

Kwa hivyo, serikali inatarajiwa kufutilia mbali taasisi zifuatazo; HELB, KUCCPS, UFB na TVETFB.

  • Tags

You can share this post!

Majuto ya Mjukuu wa Moi: Collins Kibet sasa atoweka, kesi...

Catherine, mke wa mwanamfalme William augua saratani

T L