Makala

Maadhimisho ya Idd-Ul-Fitr

April 10th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA SAMMY WAWERU

JAMII ya Dini ya Kiislamu Jumatano, Aprili 10, 2024 walikongamana katika maeneo mbalimbali ya kuabudu kuadhimisha Sikukuu ya Id-Ul-Fitr.

Sikukuu ya Id-Ul-Fitr inaashiria mwisho wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Mwezi huo ni wa tisa katika kalenda ya Kiislamu.

Sherehe za Id-Ul-Fitr huanza kwa maombi maalum yanayojulikana kama; Eid, yanayofanyika alfajiri baada ya mwezi kuonekana.

Baadaye, hushiriki karamu ya mlo na pia hualika umma kusherehekea.

Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof Kithure Kindiki kupitia taarifa alitangaza jana, Jumanne, Aprili 9, 2024 kwamba leo – Jumatano itakuwa Sikukuu kwa minajili ya maadhimisho ya Id-Ul-Fitr.

Zifuatazo ni picha za Waislamu kutoka maeneo tofauti nchini wakisali.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati wa maombi ya Eid Eldoret, Uasin Gishu yaliyoongozwa na Sheikh Mohammed Hussein mnamo Aprili 10, 2024.
PICHA|JARED NYATAYA
Waziri wa Ulinzi, Aden Duale (tatu kutoka kushoto) alipoungana na jamii ya Dini ya Kiislamu kwa minajili ya maombi ya Eid katika Uwanja wa Eastleigh High, Nairobi. PICHA|WILFRED NYANGARESI
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki maombi ya Eid katika Msikiti wa Masjid Ummu Khulthum, Kizingo, Mombasa mnamo Aprili 10, 2024. PICHA|WACHIRA MWANGI
Muumini wa Dini ya Kiislamu wakati wa maombi ya Eid Menengai Grounds, Nakuru. BONIFACE|MWANGI
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki maombi ya Eid Pamba Roho Grounds, Lamu. PICHA|KALUME KAZUNGU