• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Manufaa tumbi nzima ya tunda tamu la stroberi

Manufaa tumbi nzima ya tunda tamu la stroberi

Na DUNCAN MWERE

Wakazi wengi wa eneo la Mlima Kenya na kote nchini hawana mwao kuhusu mbinu na tija?zinazotokana na matunda aina ya stroberi.

Kwa mujibu wa wataalamu wa siha ulimwenguni, imethibitishwa kuwa matunda haya ni mojawapo ya yale yanayoweza kutibu na kuzuia magonjwa yaliyo kero?kwa jamii ya sasa.

Ni kwa sababu hii matabibu wamekuwa wakiwashauri na kuwarai wananchi kuhusu?ulaji wa matunda haya kila mara.

Ili kupata ufahamu wa kina kuhusu manufaa na taratibu za kukuza?matunda haya Akilimali ilifunga safari kwa mtaalamu aliyebobea na kupata mafanikio tele kutokana na?kilimo cha matunda ya stroberi au forosadi.

Samuel Maina Karue anayefahamika na wengi Maina?Wandare amekuwa katika zaraa hii kwa muda wa miaka 27.

Nimepata tajriba pevu kuhusu kilimo cha?storiberi kwani nilianza kukuza mnamo mwaka wa 1992, aeleza Maina katika shamba lake lililoko katika?kijiji cha Itoga Kiawarigi eneobunge la Mathira Kaunti ya Nyeri.

Kutokana na ujuzi wa miaka mingi Maina?ndiye msimamizi wa wakulima wa matunda haya japo si wengi katika janibu hii.

Aidha amekuwa akitoa?ushauri kwa wale wanaolenga kujitosa kwenye kilimo cha stroberi. Maina anashauri wakulima walio?ukanda wa Mlima Kenya kukuza mmea huu kwa wingi kwani maeneo haya hupokea mvua kwa wingi.

“?Kuna uwezekano mkubwa tunda hili kufanya vyema katika eneo hili kwani lina mito mingi na hupokea?mvua mara kwa mara,” ashauri. Kwa sasa Kenya hukuza zao hili kwa asilimia tatu pekee huku Afrika?Kusini ikiongoza barani Afrika.

Aidha anaambia Akilimali kuwa kilimo cha stroberi huhitaji sehemu ndogo?ili kukuza. Katika robo ekari ya shamba, mkulima anastahili kupanda mmea 5,000. Maina anaambia?Akilimali kuwa maji ni muhimu zaidi katika hatua zote.

Kinachofanikisha kilimo chake ni  mto kwenye shamba lake. “Bila maji mengi mkulima asitarajie kupata matunda mengi na yalio?na ubora,” aeleza.

Mbolea ya mifugo hususan ng’ombe na mbuzi ni mwafaka japo fatalaiza huanza?kutumika baada ya siku kumi tangu mmea upandwe.

Fatalaiza aina ya NPK ndio inapendekezwa na?wataalamu nyanjani. Fatalaiza hii inastahili kuongezwa kadri unavyovuna matunda yako. Katika shamba?lake yeye huvuna mara tatu kwa wiki nazo ni siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Manufaa ya tunda?aina ya storiberi ni maridhawa. Kwanza huliwa moja kwa moja likiwa tunda na hapo mtumizi huimarisha?siha yake. Pili, hutumika kutengeneza siagi ambayo aghalabu hupakwa kwenye mikate. Pia hutayarisha?sharubati.

Matumizi mengine ya stoberi ni kurembesha keki ambazo hutumika kwenye hafla za kila aina.

“Wengi wa watu hawajui matunda haya hutumika kutia nakshi katika keki,” aeleza Maina.

Licha ya?mkulima kupata ghawazi lukuki, matunda haya yanaweza kuzuia magonjwa mbalimbali. Baadhi ya?magonjwa hayo ni pamoja na saratani, kupooza (stroke), kisukari (diabetes), shinikizo la damu (blood?pressure), vimbizi au kuvimbiwa (constipation) na maradhi ya moyo.

Aidha?wataalamu wanaeleza matunda ya forosadi ni bora kwa kinamama wajazito kwani yana madini tele?yanayohitajika katika kipindi hiki.

Kutokana na utamu wa aina yake matunda haya huwa kivutio cha maadui wengi. Kuna nyuni?wanaoshambulia pindi tu yanapoiva.

Ni kutokana na sababu hii matunda haya huvunwa mara tatu kwa?wiki kwani ndege hawa hula matunda yalioiva zaidi.

Matatizo mengine yanayomkumba mkulima ni?wadudu waharibifu na magonjwa hasa ya baridi yanayochangia pakubwa mmea kunyauka.

Maina?anahimiza wakulima kusaka ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu nyanjani ili kuwa njia mahsusi za?kukabiliana na changamoto hizi kutegemea na eneo. Kuhusu soko, Maina anaeleza yeye huuzia madukaya jumla Nyeri na Kaunti ya Nairobi.

Kisiki kingine ni kuwa matunda haya?huharibika haraka, hivyo mkulima lazima ajue wanunuzi wake kabla ya kuvuna.

“Kabla ya kuwauzia?matunda lazima wahakikishe matunda ya awali yamekamilika na endapo kuna mengine yameharibika?yanarudisha kwangu hivyo kupata hasara zaidi,” afichua.

Kwa kilo moja Maina huuza kwa kati ya shilingi?100-200 kutegemea na wingi na uhaba wake sokoni. Wakati wa kongamano la magavana mwaka huu?jimboni Kirinyaga aliuza kwa wingi huku kilo moja akiuza Sh.600! Hatimaye anaeleza mkulima ambaye?atawezeka katika kilimo hiki bila shaka atakuwa ametoka kwenye lindi la ufukara.

You can share this post!

AKILIMALI: Kilimo cha mchele ndicho natija Kirinyaga

AKILIMALI: Badala ya kusubiri sana, panda tofaha hili...

adminleo