Makala

MAPISHI: Jinsi ya kuandaa nyama ya mbuzi ya kukaanga

September 25th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa kupika: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • nyama ya mbuzi kilo 1
  • beef masala kijiko 1 cha chai
  • vitunguu maji 2 vikubwa
  • nyanya 2
  • mafuta kiasi
  • pilipili mboga
  • karoti 1
  • limau 1
  • pilipili mbuzi 1
  • soy sauce
Nyama mbichi ya mbuzi. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Safisha nyama, weka kando ili ichuje maji.

Andaa vitunguu maji kwa kumenya kisha kata vipande vidogo.

Bandika sufuria mekoni. Weka mafuta ya kupikia.

Mafuta yakipata moto, weka nyama. Kaanga hadi ianze kuwa ya kahawia kisha weka vitunguu maji. Koroga na ufunike.

Saga karoti, pilipili mboga na pilipili kwa pamoja kwenye blenda.

Weka mchanganyiko huo kwenye nyama. Koroga kwa muda wa dakika tatu.

Weka soy sauce kiasi kisha koroga.

Weka nyanya, ila ni vizuri ukizisaga kwanza. Weka chumvi, kamulia ndimu kisha funika.

Hakikisha nyama inakauka na hakuna mchuzi. Weka beef masala. Koroga mpaka iwe kavu kabla ya kuepua

Pakua na chochote ukipendacho na ufurahie mlo wako.