MAPISHI: Jinsi ya kupika maharagwe yaliyotiwa manjano
Na MARGARET MAINA
Muda wa kuandaa: Dakika 15
Muda wa kupika: Dakika 30
Walaji: 3
Vinavyohitajika
- maharagwe nusu kilo yaliyochemshwa
- vijiko viwili vya mafuta ya kupikia
- kijiko kimoja cha binzari ya manjano
- kitunguu maji kimoja
- nyanya moja
- nyanya ya kopo kipimo kiasi cha kijiko kimoja
- tui ya nazi kikombe kimoja
- chumvi
Maelekezo
Weka nyanya na kitunguu kwenye blenda na utengeneze rojo.
Chemsha mafuta ya kupikia kwenye sufuria katika moto wa chini kiasi.
Ongeza rojo ya nyanya na kitunguu, binzari ya manjano na uchanganye vizuri, kisha funika mpaka iive.
Ongeza maharagwe, tui ya nazi na nyanya ya kopo. Funika tena, acha ichemke mpaka sosi iwe nzito.
Weka chumvi.
Pakua na chochote ukipendacho na ufurahie.