• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
MAPISHI: Mandazi ya unga ngano uliokandwa kwa mayai na maziwa

MAPISHI: Mandazi ya unga ngano uliokandwa kwa mayai na maziwa

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Vinavyohitajika

  • Unga wa ngano kilo 1
  • Sukari vikombe viwili
  • Chumvi kijiko 1
  • Hamira kijiko 1 kidogo
  • Mayai 2
  • Maziwa ya unga vijiko 3
  • Siagi vijiko 2
  • Hiliki kijiko 1
  • Maji ya ufufutende ya kukandia
  • Mafuta ya kupikia lita 1
  • Kibao cha kusukumia unga wa ngano
Mandazi. Picha/ Margaret Maina

Maelekezo

Weka unga kwenye bakuli kisha ongeza sukari, chumvi, mayai, maziwa ya unga, siagi na hiliki. Changanya mpaka mchanganyiko uwe sawia.

Ongeza maji ya ufufutende kiasi kwenye mchanganyiko na uanze kukanda kwa muda wa dakika 15.

Gawanya unga uliokandwa katika madonge manne tofauti.

Weka unga wa ngano kidogo katika kibao cha kusukumia na uanze kusukuma donge moja katika shepu ya chapati.

Hakikisha unga wako uko wa wastani, sio mwembamba sana wala mnene.

Ukimaliza kusukuma, kata unga kwa umbo upendalo kupika maandazi na uyatandaze katika ubao ulionyunyuziwa unga wa ngano ili kuzuia unga utakaoweka usigande.

Rudia hiyo hatua kwa madonge yote yaliyobakia.

Ukimaliza kuandaa maandazi yako, weka maandazi yako katika sehemu iliyokuwa na joto ili yaweze kuumuka kama muda wa saa tatu.

Unga ukishaumuka, bandika sufuria pamoja na mafuta ya kupikia jikoni. Hakikisha mafuta ni mengi ili kuwezesha maandazi kuiva vizuri.

Mafuta yakishachemka, tumbukiza mandazi. Acha maandazi kwenye mafuta mpaka yabadilike rangi na kuwa ya kahawia.

Maandazi yakishaiva, epua na weka kwenye chujio ili kukausha mafuta. Rudia hatua hizi kwa maandazi yote yaliyobaki.

Yakishapoa, pakua na ufurahie.

You can share this post!

Safaricom yamteua Michael Joseph kaimu Afisa Mkuu Mtendaji

Vipusa wa Uingereza roho juu wakivizia USA

adminleo