MAPISHI: Pasta na mayai
Na MARGARET MAINA
Muda wa kuandaa: Dakika 15
Mapishi: Dakika 20
Walaji: 3
Vinavyohitajika
- Vitunguu maji 2
- Mayai 4
- Pasta
- Mafuta ya kupikia
- Chumvi
- Kitunguu saumu cha unga
Maelekezo
Injika sufuria yenye maji mekoni kisha weka chumvi ya kutosha.
Weka pasta; hakikisha kwamba hujazikata katikati. Weka ziegemee upande wa sufuria kwani zikipata moto vizuri zitaingia zote kwenye sufuria.
Baada ya dakika 10 pasta zitakuwa zimeiva na kiini kimelainika.
Pasta zikiiva, toa na weka pembeni kwenye sahani.
Menya vitunguu kisha uvikate vipande vidogo. Weka kando.
Bandika kikaango (frying pan) mekoni. Weka mafuta; acha yapate moto kiasi.
Pasua mayai. Ongeza chumvi kisha koroga vizuri.
Weka kitunguu saumu na kitunguu maji kwenye kikaango.
Koroga kiasi na acha kiive kiasi.
Baada ya dakika tatu weka mayai. Tandaza vizuri. Acha yaive upande mmoja, kisha geuza vizuri upande wa pili.
Mayai yakiiva unaweza kutoa na kutenga kwa ajili ya kula.
Pakua chakula chako na ufurahie.