MAPISHI: Sambusa za mboga
Na MARGARET MAINA
Kuandaa: Dakika 20
Muda wa kupika: Dakika 20
Walaji : 3
Vinavyohitajika
- Viazi ulaya 3 vilivyochemshwa kisha uvikate vipande vidogovidogo
- Njegere (peas) zilichemshwa kidogo ½ kikombe
- Vitunguu 2 kata vipande vidogo
- Tangawizi ½
- Pilipili 2
- Bizari kijiko ½
- Giligilani iliyosagwa kijiko 1
- Garam masala nusu kijiko
- Majani ya curry 4
- Juisi ya limau kijiko 1
- Mafuta kijiko 1 cha kupikia
- Chumvi
- Karoti 2; katakata
- Unga wa ngano vijiko 4 au ute wa yai
- Chapati dough
Maelekezo
- Kwenye kinu, weka tangawizi, kitunguu saumu na pilipili. Twanga kwa pamoja hadi vilainike kisha hifadhi pembeni.
- Bandika sufuria au kikaangio jikoni. Weka mafuta, yakipata moto weka, bizari na majani ya curry. Pika kwa dakika 2 huku ukigeuza mara kwa mara. Weka mchanganyiko wa pilipili kisha pika hadi harufu ya kitunguu saumu na tangawizi ipotee.
- Weka kitunguu maji, pika kwa dakika mbili kisha weka mboga yoyote ya majani utakayopenda.
- Weka viazi ulaya, unga wa giligilani, bizari, garam masala na chumvi. Changanya vizuri mpaka viazi vichanganyikane na viungo vingine.
- Punguza moto uwe wa wastani, pika kwa dakika tano huku ukikoroga taratibu. Weka njegere na limau. Changanya vizuri kisha pika kwa dakika mbili hivi. Toa motoni na acha mboga zipoe kabisa.
- Koroga unga wa ngano au ute wa yai, hii itakusaidia kufungia sambusa.
- Kata manda kwenye umbo la pembetatu kisha weka mboga mboga kiasi. Anza kufunga ila ukifika mwisho paka ute wa yai au unga wa ngano uliokoroga. Inasaidia sambusa zisifunguke wakati wa kupika.
- Bandika kikaango chenye mafuta jikoni. Mafuta yakipata moto anza kupika sambusa hadi zigeuke rangi na kua kahawia. Yatoe na hifadhi pembeni. Rudia hii hatua hadi sambusa zote ziive.
Sambusa zikishapoa, pakua na ufurahie na wenzako.