MAPISHI: Scones zilizotiwa juisi ya limau
Na MARGARET MAINA
MUDA wa kuandaa: Dakika 15
Muda wa mapishi: Dakika 20
Walaji: 4
Vinavyohitajika
- sukari nusu kikombe
- kijiko 1 cha maganda ya limau
- vikombe 3 unga wa ngano
- baking powder kijiko 1 cha chakula
- chumvi kiasi cha robo tatu ya kijiko
- cream cheese kiasi cha robo kikombe
- vijiko 6 vya siagi (unsalted butter)
- mayai 2
- maziwa nusu kikombe
- kijiko 1 cha juisi ya limau
Maelekezo
Washa ovena na dhibiti kiwango cha joto kiwe ni nyuzijoto 200. Acha ipate moto. Kwangua maganda ya limau na kukamua maji yake.
Katakata siagi iwe vipande vidogovidogo.
Kwa kutumua vidole vyako, changanya uwe kama unasugua sukari na maganda ya limau mpaka ichanganyike vizuri na ilainike.
Ongeza unga wa ngano, baking powder na chumvi. Changanya vizuri.
Katika bakuli jingine, saga cream cheese, siagi na mayai kisha changanya vizuri.
Ongeza mchanganyiko kwenye bakuli lenye unga wa ngano, pamoja na maziwa na juisi ya limau.
Kanda unga mpaka ulainike, kisha katakata kama utakavyopenda.
Oka scones kwenye chombo cha kuokea kwa robo saa.
Acha zipoe kwenye waya wa kupozea chakula.
Wakati zinapoa, changanya icing sugar, maji ya limau na maganda ya limau mpaka upate mchanganyiko mzuri.
Nyunyizia mchanganyiko wa icing sugar juu ya scones.
Pakua na ufurahie.