Mbwembwe, shangwe na nderemo kwa walimu wa Shule ya Msingi ya Wasichana ya Lokichar wakipokea tuzo katika mashindano ya kitaifa za muziki yanayoendelea katika Chuo cha Walimu cha Meru. Picha|Tobbie Wekesa
MASHINDANO ya Kitaifa ya Tamasha za Muziki yanayoendelea katika Chuo cha Walimu cha Meru yanazidi kutia fora huku mawasilisho mbalimbali yakisisimua wadau.
Mashindano ya mwaka huu yameonyesha ubunifu wa hali ya juu huku wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali wakizidi kuonyesha umarufu na vipaji vyao.
Tazama mambo yanavyoendelea, kwa picha….
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Hill School kutoka Eldoret wapiga pozi katika Shule ya Upili ya Kaaga, Meru.
Wanafunzi wa Chuo cha Walimu cha Kamwenja Jukwaani.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Elegant Spur kutoka Ruiru.
Wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi ya Damacrest kutoka Kiambu wakisherehekea tuzo baada ya ushindi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kivaywa jukwaani.
Shule ya St Michael Shamusinjiri kutoka Ikolomani, Kakamega. PICHA ZOTE|TOBBIE WEKESA