Makala

Mfanyabiashara katika duka la jumla akana kuiba Sh296M

Na RICHARD MUNGUTI January 6th, 2026 Kusoma ni dakika: 2

MFANYAKAZI katika duka la jumla ameshtakiwa kuiba Sh296 milioini katika muda wa miaka saba kati ya 2018 na 2025.

Mohamed Osman Abdile ambaye pia anamiliki kampuni ijulikanayo kwa jina  Fatzam Enterprises Limited (FEL) anadaiwa na kiongozi wa mashtaka ya umma (DPP) kwamba alificha kabisa kule alikopata pesa hizo.

Mahakama imeelezwa na DPP kwamba Abdille anayeshtakiwa pamoja na FEL alikuwa ameweka  pesa hizo kwenye akaunti za Benki za Kenya Commercial Bank (KCB), Absa Bank na Equity Bank Limited (EBL) matawi ya Eastleigh County ya Nairobi.

Mshtakiwa , mahakama iliambiwa alikataa kufichua alikotoa zaidi ya Sh116milioni ambazo polisi walikuta kwenye akaunti zake katika mabenki ya KCB, Absa na EBL.

Pia mshtakiwa alikataa kata kata kwamba Sh107milioni alizokuwa nazo zilikuwa zimpetikana kwa njia isiyo halali.

Alikana alijua pesa alizokuwa ameweka katika akaunti za benki hizo zilikuwa sehemu ya Sh296,069,084 zilizoibwa kutoka kwa Bw Abid Mohamed Ali kati ya Januari 1 2018 na Feburuari 19,2025.

Mahakama ilielezwa kwamba wakurugenzi wawili wa FEL-Mabw Abdille na Hussein Ibrahim Barre ambaye hakufika kortini kujibu mashtaka walificha kabisa kule pesa hizo zilitoka kwa kuagiza Spaghetti ya mamilioni ya pesa kutoka kampuni ya Arabian Milling & Food Company.

Mbinu nyingine ambazo Abdille, Barre na FEL wanadaiwa walitumia kuficha pesa ni kuzihamisha na kuweka katika akaunti za makampuni ya Gigi International Limited, Marray and Sons Venture Limited, Arabian Milling & Food Company, Ada Food Gida Sanayive Tlc, Ismail Mohamed Ali na Hussein Ibrahim Barre.

Bw Abdille alikabiliwa na mashtaka 30 ya kula njama za kutekeleza uhalifu, wizi, kuficha alikotoa pesa na kuzihamisha kutoka akaunti ya FEL hadi kwa akaunti nyingine.

Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kwamba Abdille aliiba Sh296,069,084 kati ya Januari 1,2018 na Septemba 30 2024.

Abdille anadaiwa alitekeleza uhalifu huo pamoja na FEL.

Katika mashtaka ya kuficha pesa kwenye akauntu Abdulle ameshtakiwa pamoja na mkurugenzi mwenza katika FEL Bw Hussein Ibrahim Barre ambaye hakufika mahakamani kujibu mashtaka.

DPP aliambia mahakama pesa anazodaiwa kuiba Abdille zilikuwa za Abdi Mohamed Ali.

Mshtakiwa alidaiwa alipata pesa hizo kutokana na kazi yake alipokuwa ameajiriwa katika Mega Shopping Mall.

Abdille na FEL walikana kwamba kati ya Januari 1,2018 na Septemba 30,2024 waliiba Sh296.089,084 zake Abdi Mohamed Ali.

Mnamo Machi 12, 2024 Abdille alikutwa ameweka Sh4,759,029 akijua zilipatikana kwa njia isiyo halali.

Pesa hizo zilikuwa kwenye akaunti FEL katika benki ya KCB.

Polisi kutoka kitengo cha kupambana na uhalifu kwenye mabenki (BFU) cha Benki Kuu ya Kenya (CBK) kiligudua zaidi Sh116milioni kwenye akaunti za FEL,

Pia Abdille na Barre hawakuweza kueleza jinzi walijipatia Sh107,359,527.

Abdille alikana mashtaka 30 na kuomba aachiliwe kwa dhamana akisema “hatatoroka ila atafika kortini wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo.”

Aliongeza kusema ameekeza mali mengi nchini na hawezi kutoroka aiache.

Upande wa mashtaka haukupinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Mahakama ilimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh3milioni na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.

Pia aliagizwa alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh2milioni afanye kesi akiwa nje.

Kesi itatajwa baada ya wiki mbili  kwa maagizo zaidi.