• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 6:21 PM
Mradi wa mikoko Kwale wasaidia katika uhifadhi wa mazingira

Mradi wa mikoko Kwale wasaidia katika uhifadhi wa mazingira

Na MAGDALENE WANJA

KAMA nchi zingine, Kenya hukumbwa na changamoto tele ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Uchafuzi huu huwa na madhara ya kiafya kwa binadamu na huchangia sana katika maradhi yanayotokana na hewa chafu.

Kulingana na Wizara ya Afya, Wakenya 13,000 hufariki kila mwaka kutokana na maradhi yanayohusishwa na hewa chafu.

Miji mikuu ndio imeathirika zaidi na janga hili ambalo kwa asilimia kubwa limesababishwa na binadamu ambapo kiwango kikubwa cha hewa aina ya kaboni huachiliwa kwenye hewa.

Hata hivyo kikundi kimoja katika kaunti ya Kwale, kimeanza kujikimu kimaisha tangu mwaka 2013 kutokana na upanzi wa miti aina ya mikoko.

Mradi huo kwa jina Mikoko Pamoja umeleta pamoja jamii mbili katika eneo la Gazi Bay.

Kulingana na msimaizi wa mradi huo Bw Josephat Mwamba, hii ni mojawapo ya miradi ya aina hiyo ya gesi ambayo imefaulu.

“Tunapata Sh 100,000 kila mwezi kwa kutunza msitu na kupanda miti aina ya mikoko,” anasema Bw Mwamba.

Msimamizi wa mradi huo Bw Josephat Mwamba aonyesha jinsi ya kupima miti ya mikoko. Picha/ Magdalene Wanja

Kutokana na kufaulu kwa mradi huo, serikai ya Ufaransa inasaidia katika utunzaji wa mikoko katika maeneo ya Pwani ya Kenya kwa kutoa Sh114 milioni.

Kulingana na msimamizi mkuu wa huduma ya KFS Bw Julis Kamau, Kenya tayari imepoteza hekari 17 za msitu wa mikoko kutokana na ukataji miti, ongezeko la maji ya chumvi na uchafuzi wa mazingira.

“Uharibifu huo pia umechangiwa na ongezeo la idadi ya watu katika maeneo ya pwani hali inayosababisha katika ongezeto la upepo katika maeneo hayo,” akasema Bw Kamau.

Bw Kamau anaongeza kuwa Kenya ina hekari 60,645 za mikoko ambazo zinapatikana katika eneo la umbali wa kilomita 536 kando ya bahari na asilimia 60 iapatikana katika Kaunti ya Lamu.

Wakazi wa Gazi katika kaunti ya Kwale wanategemea uvuvi kwa kiwango kikubwa kujikimu kimaisha.

Kama njia mojawapo ya kuzuia uharibifu wa missitu, wameweza kupanda miti aina ya Casuarina amabyo inatuika kama kuni badala ya mikoko.

Kupitia mapato hayo, wakazi wa Gazi wameweza kuinuka kimaisha na wameweza kupata stima na maji.

“Hatukuwa na maji safi lakini kufikia sasa tuna maji ya mfereji na stima pia kupitia mapato ya mradi hu,” anasema Mama Hafsa ambaye ni mkazi wa eneo hilo.

You can share this post!

Wafanyakazi waliouza umeme wa Kenya Power kwa bei nafuu...

Yatani aahidi kutekeleza Ajenda Nne Kuu

adminleo