Msingi wa umoja uliowekwa na Nyerere unavyotishiwa na misukosuko ya sasa TZ
KWA miongo kadha Tanzania imetambuliwa kama taifa lenye utulivu katika bara la Afrika.
Huku nchi jirani zikikumbwa na misukosuko inayosababishwa na mapinduzi pamoja na uchanguzi yenye matokeo ya kubishaniwa, Tanzania imesalia tulivu huku wananchi wakidumisha umoja kutokana na maono ya rais wake wa kwanza Julius Nyerere.
Leo hii sura hiyo imeharibiwa. Nchi iliyosifiwa kama kitovu cha amani sasa ni taifa lenye kafyu na maafa yanayotokana na machafuko ya uchaguzi.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yanakadiria kuwa zaidi ya watu 700 wamekuwa katika ghasia zilishuhudiwa haswa Tanzania bara siku ya uchaguzi, Jumatano wiki jana.
Mamia ya watu hawajulikani waliko huku wengine wakiwa wamezuiliwa katika korokoroko za polisi bila kufunguliwa mashtaka.
Barabara za miji mbalimbali, ambazo zamani zilisheheni uchangamfu na biashara sasa zimesheheni hofu na taharuki.
Kwa raia wengi wa Tanzania bara, shida nchini humo ni zaidi ya siasa.
Raia wanahisi kupokonywa haki yao.
Japo Nyerere alipalilia hisia ya usawa mnamo 1964, wakati huu raia wa Tanzania bara wanahisi kudhibitiwa na Zanzibar.
Zanzibar ndio inaongoza na wao wanatakiwa kutii.
Tanzania ilipopata uhuru wake mnamo 1961, ndoto ya Nyerere ilikuwa kujenga Jamhuri iliyoshikanishwa na malengo ya pamoja wala sio ukabila na ulafi.
Alionya kuwa mashindano kati ya vyama vya kisiasa yangevuruga umoja wa Tanzania.
Chini ya chama cha Tanganyika African National Unioni (TANU) Nyerere alijenga kila ambacho alikiita “demokrasia shirikishi” chama kimoja, watu wamoja walioelewana.
Tanganyika iligeuka kuwa kisiwa cha utulivu kilichozingirwa na nchi zilizozongwa na machafuko.
Kisha ikaja Zanzibar.
Mnamo 1964, baada ya kisiwa hicho kuzongwa na maasi yaliyoongozwa na vuguvugu la Afro-Shirazi waliopania kuondoa mamlakani utawala wa Kiarabu, Nyerere na kiongozi wa Zanzibar wakati huo Abeid Amani Karume walitia saini Mkataba wa Muungano uliozaa Muungano wa Tanzania.
Ilikuwa ni ndoa yenye umuhimu sio wa “kimapenzi”
Chini ya mkataba huo, Zanzibar alisalia na Rais wake, Bunge na Idara ya Mahakama lakini Tanzania bara iligeuka kuwa injini ya muungano huo—ikiajiri wanajeshi, maafisa wa serikali na kusimamia shughuli nyingi za kiuchumi.
Japo kwa maneno, washirika hao wawili walikuwa sawa; lakini kiutendeti mamlakani nyingi ilikuwa Dar es Salama, mji mkuu wa Tanzania bara.
Mnamo 1977, TANU iliungana na chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kilichoonza kama muungano wa kisiasa uligeuka kuwa wa kiitikadi.
“Serikali ni chama na chama ni Serikali,” Nyerere alitangaza.
Lakini umoja huu ulikuwa na faida na hasara yake. Japo utawala wa chama kimoja ulilenga kudumisha umoja, kuliibuka malalamishi ya chini kwa chini kisiwani Zanzibar na hata Tanzania bara.
Kufikia 1980, ufa ulianza kupanuka zaidi. Rais wa Zanzibar wakati huo Aboud Jumbe alipojaribu kupendekeza mageuzi ili kugeuza serikali ya Muungano kuwa wa Majimbo, Nyerere alizima juhudi hizo.
Jumbe alifurushwa CCM mnamo 1983 na kupokonywa mamlaka.
Baada ya Nyerere kustaafu mnamo 1985, Ali Hassan Mwinyi, raia mwingine wa Zanzibar, alitwaa wadhifa wa Rais wa Tanzania.
Wimbi la mageuzi yalipoanza kuvuma bara la Afrika katika miaka ya 1990s, Tanzania haikusazwa.
Hatimaye mnamo 1992, siasa za vyama vingi ziliruhusiwa nchini humo.
Katika Tanzania bara, kulichipuka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na katika Zanzibar kukaundwa chama cha Civic United Front (CUF) kilichopigania uhuru na uwajibikaji.