Mulamwah motoni kuzua kiki ya talaka
MCHEKESHAJI Kendrick Mulamwah katolewa povu na mastaa wenzake kwa kile wanachohisi tangazo lake la kuachana na demu wake Ruth K ni kiki ya kupromoti shoo yake ijayo.
Juzi Mulamwah alitangaza kuwa ameachana na Ruth K ikiwa ni siku chache kabla ya shoo yake ya ‘I can Explain’ iliyoratibiwa kufanyika Aprili 20.
Baada ya kutoa tangazo kuwa wameachana kufuatia kuibuka kwa uvumi kuwa hawapo pamoja tena, baadhi ya maceleb waliamua kumvaa.
“Wacha hizo wewe Ruth ni wewe na wewe ni Ruth kesi imeisha, acha vipindi,” alimchamba Chris Kirwa.
Naye staa Milly Chebet aliamua kumpa ushauri, “Tulia kaka hauhitaji vipindi, shoo itajaa wewe tuwekee linki tununue tiketi tukusapoti, hizi kelele haziwezi.”
Skinnuy Shinski naye vile vile akampa makavu, “Wacha presha mzee, shoo tutakuja sio lazima hizi kiki.”