• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
Namna asili ya kuondoa vichwa vyeusi ngozini (blackheads)

Namna asili ya kuondoa vichwa vyeusi ngozini (blackheads)

Na MARGARET MAINA

[email protected]

BLACKHEADS ni aina ya chunusi ambazo hutokea baada ya kuongezeka kwa mafuta ya ngozi au seli zilizokufa.

Katika kuongezeka huku kwa sebum na seli za ngozi zilizokufa, kijitundu ngozini kitakuwa wazi, hali inayoitwa open comedone au blackhead itatokea.

Kuzidi kuongezeka kwa mafuta kutoka sebaceous glands, kutalifanya eneo linalokizunguka kijitundu cha kinyweleo kuvimba. Blackheads zinaweza kuambatana na mashambulizi ya bakteria endapo wataweza kushambulia eneo linalozunguka kijitundu cha kinyweleo.

Tumia pilipili manga na maziwa mtindi kuondoa blackheads yaani “vichwa vyeusi”.

Unahitaji

  • maziwa mtindi kiasi cha vijiko 2
  • kijiko 1 cha pilipili manga (ya unga ni bora zaidi)

Muda wa kuandaa: Dakika 1

Maelekezo

Changanya hivi vitu vyote unavyovihitaji kwenye bakuli safi.

Osha uso wako; uache ukauke kidogo tu.

Paka mchanganyiko wako usoni na shingoni.

Sugua taratibu kwa kuzunguka kwa robo saa.

Osha na maji ya uvuguvugu na ujikaushe (Ni muhimu utumie kiwiko kupima joto la maji ili yasikuchome).

Pilipili manga ina uwezo wa kuongeza mzunguko wa damu kwenye ngozi yako ya uso, hivyo basi mzunguko wa hewa safi pamoja na virutubisho huongezeka.

Vile vile inazuia bakteria hatari wasiingie kwenye ngozi yako. Bakteria huleta chunusi aina ya blackheads “vichwa vyeusi”.

Maziwa mtindi yana lactic acid na yenyewe inaweza kutoa ngozi iliyokufa “dead skin” na kupunguza ukubwa wa tundu za uso na kung’arisha uso wako na kuua bakteria hatari huku ikikuachia bakteria nzuri.

You can share this post!

LISHE: Namna ya kuandaa mboga mchanganyiko

Mwokaji ambaye makuza ya nchini Kenya na Afrika Kusini...