
Shugamami akiwa na kijana barobaro. PICHA|HISANI
SWALI: Kwako shangazi. Nimevutiwa kimapenzi na mwanamke ambaye amenizidi umri kwa miaka kumi.
Nia yangu hasa ni kumuoa kwa sababu nimeona anatosha kuwa mke wangu. Nahitaji ushauri wako.
JAWABU: Hali kwamba umeamua kumuoa mwanamke ambaye amekuzidi umri kwa miaka hiyo ni ishara kuwa unampenda kwa dhati na hilo hasa ndilo jambo muhimu katika ndoa.
Kama yeye pia hana shida na hali hiyo, hakuna kitu au mtu wa kuwazuia.