
Mume akilia baada ya mkewe kulala nje ya ndoa. PICHA|HISANI
SWALI: Kwako shangazi. Nimegundua mpenzi wangu alihama kwake ghafla bila kuniambia.
Ajabu ni kuwa amehamia kwa mwanamume rafiki yangu. Jambo hilo limenishangaza na kuniumiza sana moyoni kwani sijawahi kuwashuku. Nifanyeje?
JAWABU: Hatua ya mpenzi wako ya kuhamia kwa rafiki yako inaonyesha wazi kuwa amemchagua yeye.
Ameamua iwe hivyo na huwezi kumlazimisha aendelee kukupenda. Kubali uamuzi wake na uendelee na maisha yako.