Fanya hivi kudumisha mnato katika ndoa
KUNA baadhi ya mambo ambayo wake na waume huwa wanahitaji kutoka kwa wachumba wao ambayo wengi huwa wanawanyima kwa kusudi au kutojua.
Ni vyema kwa mume, kutambua kuwa mkeo ni ni mpenzi; si mke tu, na hivyo ni muhimu kuonyesha upendo wako kwake. Mpende kwa moyo wako wote. Mwanamume yeyote anayemjali mkewe afaa kufahamu hili na kulikumbatia.
Vile vile, mkeo ni rafiki yako, mtumainie, mlee, mfurahie, omboleza naye, msherehekee na zaidi cheka naye. Mtendee kama mtoto mchanga, mlishe na umthamini. Mruhusu alale kifuani mwako, mbembeleze na umruhusu ajisikie vizuri na wewe.
Utakuwa unakosea kwa kumtenga kwa visingizio vingi vya hapa na pale. Kaa na mkeo uliko ikiwezekana, mlale kwenye kitanda kimoja, mfanye awe na ahisi raha ya kuwa mwenzi wako.Kumbuka kuwa mkeo ni mwenzi wako wa roho, mpe akili yako na moyo wako, usimfiche chochote. Mtambue kama malkia wako.
Mke wako ni mshirika wako wa ngono; usione aibu kufanya naye mapenzi. Mvue nguo, jifurahishe, hakikisha naye anaifurahia. Usiwe mchoyo, mtazame usoni, na uangalie ikiwa anaifurahia.
Usilale na mwanamke mwingine yeyote, ni dhambi.Mume astahili kumheshimu mkewe kama malkia jinsi alivyo; ukifanya hivyo, atakutendea kama mfalme. Ikiwa wewe ni mfalme, zungumza naye kwa heshima.
Ndoa iliyokitwa kwa msingi wa heshima haiyumbi.Kufanya hivi, mkeo anapaswa kuwa mwanamke wa pekee kwako, mwanamke nambari moja maishani mwako. Kamwe usiruhusu mwanamke mwingine yeyote, mama yako, dada zako au wafanyakazi wenzako kuchukua nafasi yake katika maisha yako.Mfundishe mkeo kile unachotaka afanye.
Usimkasirikie; mwache aendelee kujifunza kwako, wewe ni mwalimu wake namba moja.Vilevile, wanawake wanastahili kufahamu kuwa hakuna mwanamume mgumu, ujinga ndio huleta ugumu.
Ukitaka mwanaume akupende, lazima uelewe ni nini kinamfanya awe mwanaume.Wanawake wengine wanatarajia wanaume wao kukubali ushauri wao wote na kufuata maagizo yao yote, hiyo haiwezekani!
Hawezi kukubali kila kitu. Yeye ndiye kichwa. Hauwezi kulazimisha mawazo yako kwake, unaweza kushauri tu, uamuzi wa mwisho upo mkononi mwake.Wanaume hutaka amani.
Ugomvi, kupiga kelele, matusi na kumlaani kunaweza kumkosesha utulivu.Wanaume wengine huchukia kurudi nyumbani mapema kwa sababu ya usumbufu wa wake wao. Wanaume hukimbilia wanawake wanaowapa amani si kuwavunja vipande vipande kwa kelele na ubishi.Wanaume pia hupenda mlo bora.
Akikupa pesa za chakula, anataka mlo unaoakisi pesa hizo! Ongeza kile ulicho nacho, mpikie kama mfalme na atakwama kwako.Na usisahau kusifu mume wako dada. Wanaume wanapenda kumiminiwa sifa na wake wao.