• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Safisha nywele: Wigi si za kuficha nywele chafu, upara

Safisha nywele: Wigi si za kuficha nywele chafu, upara

NA PAULINE ONGAJI

ATHARI zinazotokana na kusonga na kupaka nywele dawa za kuzilainisha, zimesababisha mabinti wengi kuanza kuota upara.

Kutokana na hili, wengi sasa wamefanya uamuzi wa kunyoa nywele zao angalau kuzipa nafasi ya kupumua na kukua vyema.

Ili kufanikisha haya na kudumisha mwonekano, sasa wengi wanavalia nywele za kubandika al-maarufu wig au wigi kwa Kiswahili, hasa wakiwa na shughuli rasmi. Lakini hata wanapofanya hivyo, hawapaswi kusahau nywele zao halisi ndani ya kofia hizo. Ili kutunza nywele zako halisi wakati huu:

Osha nywele zako:

Ni muhimu kuhakikisha kuwa nywele zako ni safi hata ikiwa umevalia nywele za kubandika. Kutokana na sababu kichwa chako kitasalia kimefunikwa kwa muda mrefu, kuna uwezekano wa jasho kujikusanya na hata kusababisha harufu mbaya.

Kwa hivyo safisha nywele zako angalau mara moja kwa wiki.

Paka nywele zako mafuta:

Nywele hizi za kofia zina uwezo wa kufyonza unyevu kwenye kichwa chako na hivyo unashauriwa kupaka nywele zako mafuta angalau mara kadha kila wiki. Pindi unapofika nyumbani, ondoa kofia hiyo kisha upake mafuta.

Tenganisha nywele zako na uzisonge:

Ikiwa nywele zako ni ndefu na zaweza kujikunja basi itakubidi kuzitenganisha na kuzisonga kabla ya kuvalia kofia hii ya nywele za kubandika.

Mwanamke akichana nywele zake. PICHA | MAKTABA

Mbali na kupunguza matuta unapovalia kofia yako, mbinu hii itazuia nywele zako zisichanike kutokana na mgusano wa kila mara na kofia yako.

Shughulikia ngozi ya kichwa chako:

Usipuuze kichwa chako eti kwa sababu umevalia nywele za kubandika kwaweza kusababishia madhara kama vile ngozi kukauka na kuasha na hata kichwa chako kuvunda. Paka mafuta ya kuzuia ngozi kukauka na kukabiliana na maambukizi ya ukuvu. Hii itasaidia nywele zako kusalia na afya na kuzuia bakteria hatari kuota kwenye kichwa chako.

Patia kichwa chako nafasi ya kupumua:

Japo unavalia kofia yako kila mara, itakuwa vyema iwapo wakati mwingine utaacha kichwa chako kikae hivyo angalau kipate muda wa kupumua.

  • Tags

You can share this post!

Ufisadi: Hofu mabilionea wa mafuriko waja ilivyokuwa wakati...

Mabalozi 26 wapya sasa kuanza kazi baada ya kuteuliwa rasmi...

T L