Mteja akitumia simu ya mkono. PICHA|PEXELS
SWALI: Kwako shangazi. Nimekuwa na mpenzi kwa miezi kadhaa na nampenda kwa moyo wangu wote. Lakini kuna dalili zinazonitia hofu. Ameanza kunihepa. Anapuuza simu zangu na nikitaka tukutane ananipa vijisababu. Nifanye nini?
Jibu: Mapenzi ni maua. Huchanua na pia kunyauka. Kama mpenzi wako ameamua kukuacha huwezi kumzuia. Yeye si mke wako na hata mke wako anaweza kuamua ametosha ndoa na kuondoka. Iwapo ameamua hivyo, itabidi ukubali uamuzi wake.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO