Shangazi Akujibu

Amehepa baada ya kupata kazi, nina mimba yake

Na SHANGAZI November 17th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Kwako shangazi. Mimi na mpenzi wangu tumepitia hali ngumu ya maisha kwa kukosa kazi na hali hiyo haijaathiri uhusiano wetu. Sasa amenigeuka baada ya kupata kazi. Ananiambia ana mke ilhali nina mimba yake. Nifanye nini?

Jibu: Mpenzi wako anatumia hicho kama kisingizio tu kwa sababu anahofia utamtegemea kwa mahitaji yako. Pili, umekosea kupata mimba yake ilhali huna kazi. Itabidi ubebe mzigo huo peke yako.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO