Shangazi Akujibu
Huyu binti amejaa kiburi sababu ni mrembo mno
HUJAMBO Shangazi?
Kwa miezi mwili nimekuwa nikijaribu kumrushia mistari binti huyu mtaani. Yeye ni mrembo sana na amekuwa kivutio kwa akina kaka wengi.
Licha ya jitihada zangu za kutaka kumnasa amekuwa akinipuuza na hata wakati mwingine kunionyesha dharau kupitia jumbe zake. Nifanyeje?
JIBU: Sijambo! Anayokuonyesha binti huyu ni ishara tosha kwamba hana haja nawe.
Usijikosee heshima kwa kuendelea kumfuata mtu ambaye hana haja nawe.