Shangazi Akujibu

Mke wangu asema sijui kumuonyesha mapenzi

Na SHANGAZI October 29th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Shikamoo shangazi. Mke wangu anasema siko romantic na sijui kuonyesha mapenzi. Anadai mimi ni millennial. Je, haya mambo ya maua na picha mitandaoni ndiyo kipimo cha mapenzi siku hizi?

Jibu: Mapenzi si maua wala ‘selfie’ mitandaoni. Ni kuheshimiana, kusaidiana na kuonyesha upendo katika vitendo. Mwambie herufi R ya romantic isiishie kwenye roses, bali responsibilities.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO