Mpenzi amenikazia asali akidai wakati bado, ananipenda kweli?
Kwako shangazi. Nampenda mpenzi wangu hasa kwa sababu tumekuwa tukisaidiana kwa hali na mali. Tatizo pekee ni kuwa amekataa kabisa nilambe asali akisisitiza wakati bado. Ananipenda kweli?
Usimlazimishe mpenzi wako kufanya jambo lolote. Mapenzi ya dhati yanafaa kuwa na subira. Unasema mnampendana na mnashirikiana kwa mambo yote. Tosheka kwa hayo sasa hadi atakapokuwa tayari kwa hayo mengine.
Yake ni magumu, kila nikimpigia simu anakata akiahidi kunipigia baadaye
Kwako shangazi. Nina mpenzi na nimekuwa nikimpa chochote anachotaka. Lakini ameanza tabia ambayo sielewi. Nikimpigia simu anakatiza akiahidi kunipigia baadaye. Nikimtumia jumbe pia anapuuza. Nina hofu, nishauri.
Tabia ya mpenzi wako ni ishara kwamba hakutaki tena katika maisha yake lakini anashindwa kukwambia. Itakuwa vyema umuulize mpango wake hasa ili usiendelee kupoteza wakati na pesa zako kwake.
Anadai alikosana na mkewe akamuachia nyumba, hiyo inawezekana?
Kwako shangazi. Mpenzi ameniambia anataka kunioa. Alikuwa ameoa lakini akakosana na mkewe wakaachana. Alimuachia nyumba yao na sasa anaishi katika nyumba ya kupangisha. Je, hiyo ni kawaida?
Mume anafaa kuwa mwenye nyumba anamoishi na familia yake. Kama mpenzi wako amekubali kumuachia mkewe, inawezekana si yake. Hiyo ina maana akikuoa mtaishi nyumba ya kupangisha hadi atakapotafuta nyingine.
Nahisi pia ananipenda lakini hasemi kitu!
Shangazi naomba ushauri wako., Moyo wangu umetua kwa mwanamke tunayefanya kazi pamoja. Nina hakika yeye pia ananipenda lakini hajawahi kuniambia. Ni kwa nini?
Sijui ulijuaje kuwa mwanamke huyo anakupenda. Iwapo hajakwambia na unaamini tu anakupenda, basi unajidanganya. Kwa nini usimuulize ili upate ukweli kutoka kwake badala ya kuendelea kuota?