Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Mpenzi wangu ananichunga sana
Wanandoa wanaofaragana. Picha|Maktaba.
SWALI: Mpenzi wangu hataki niongee na marafiki na hataki nitoke bila ruhusa yake. Anasema ananipenda sana ndiyo maana. Je, haya ni mapenzi ya kweli?
Jibu: Upendo haupaswi kuwa kama gereza. Mtu anayekupenda anakupa uhuru, si maelekezo ya kijela. Kimbia kabla hajaanza kukufungia simu na kufukuza marafiki zako.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO