Shangazi Akujibu

Mume wangu amezamia majukwaa ya kusaka wapenzi mitandaoni!

Na SHANGAZI October 30th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SWALI: Kwako shangazi. Nilishtuka kumkuta mume wangu akiwa na akaunti ya kutafuta wachumba mtandaoni. Anasema ilikuwa mzaha tu. Je, nimwamini?

Jibu: “Mzaha” wa kutafuta wachumba si mzaha, ni usaliti. Kama kweli hana kitu cha kuficha, aifute mbele yako. Ukiona anasitasita, jua moyo wake una wavu wa sumu.

IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO