Shangazi Akujibu
Nilimsamehe mume ila anaendelea kunichiti
SWALI: Vipi shangazi. Mume wangu alinisaliti mwaka jana na tukamaliza tofauti zetu, lakini sasa anaanza tena kuzungumza na mwanamke aliyetukosanisha kisiri. Je, niendelee kuvumilia?
Jibu: Pole lakini anayekusaliti mara moja na akose kubadilika ni ishara ya madharau. Usipoteze muda kumlinda mtu ambaye hataki kulindwa. Uaminifu si zawadi ya kuombwa, ni uamuzi wa moyo. Kama unaona dalili zilezile, jitayarishe kujilinda kiakili na kihisia.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO