Shangazi Akujibu
SHANGAZI AKUJIBU: Anadai wanaongea na ex kuhusu watoto, hii ni kweli au nitakuja kujuta
Mwanaume anayechiti mpenzi wake. Picha|Maktaba.
SWALI: Hujambo shangazi. Nilimpata mume wangu akiongea kwa sauti ya chini na ex wake usiku. Alisema alikuwa anamuuliza jinsi watoto wanavyoendelea. Je, hii ni ishara ya usaliti?
Jibu: Sielewi kwa nini huyo waliyeachana apige simu usiku. Hii ni ishara unayostahili kuifuatilia kwa makini na kuweka mipaka mapema kuhusu heshima na kinachostahili kufanyika.
IMETAYARISHWA NA WINNIE ONYANDO